Serikali yaja na Mfumo wa Kudhibiti Michezo ya Kubahatisha
08 Oct, 2024

Kutokana na wimbi la vijana wengi kujihusisha na michezo ya kubahatisha na kusahau majukumu ya ujenzi wa taifa, Serikali ikishirikiana na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imebuni na kutengeneza mfumo maalum ambao utatumika kudhibiti uchezaji wa michezo hii (Responsible Gaming). Pia, Mfumo huu utatumika kudhibiti udanganyifu ambao unafanywa na waendeshaji wa michezo ya kubahatisha ili Serikali ipate mapato yake halali.
https://mobile.mwananchi.co.tz/Habari/Waziri-Mpango-aelezea-mikakati-ya-kuiboresha-TRA/1597580-5156322-format-xhtml-m8wsj5/index.html