Sekta Ya Michezo Ya Kubahatisha Inakua Kwa Kasi - Mkurugenzi Mkuu Wa GBT

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe sekta ya michezo inakua na kuchangia maendeleo ya kiuchumi. Mbalwe ameyasema hayo wakati wa kikao cha Wahariri na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Amesema michezo ya kubahatisha ni michezo kama mingine na hakuna nia kutaka vijana waharibiwe. Mbalwe amesema kuwa mchezo wa kubahatisha baadhi wamekuwa wakinyanyapaa na kutaka kuwa GBT ipo kisheria na inadhibitiwa. Amesema kuwa katika kodi yamepanda kutoka kodi Bilioni 33.3 hadi kufikia kodi bilioni ya 170.4 na wanatarajia kukusanya kodi ya bilioni 200 kwa mwaka wa fedha unaoishia 2023/2024. Amesema katika ushirikiano usimamizi na udhibiti wa sekta na vyombo Ulinzi na Usalama y ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya kubahatisha nchini.
Amesema wanaona umuhimu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa vile GBT ni taasisi kwa miaka 20 hivyo wajibu. Alisema semina hizi na watu muhimu wa vyombo vya habari kama hizo zimekuwa na manufaa makubwa katika kurahisisha utendaji wa GBT. “Kazi yetu ni udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na haifanyi biashara na iko chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina.” Alifafanua Bw. Mbalwe alimeelezakuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa sekta na hivyo tunaomba kamati ya usalama ya mkoa kuongeza ushirikianoz aidi katika kudhibiti wavunja sharia ya Michezo ya Kubahatisha. “Nina sisitiza Michezo ya Kubahatisha ni Burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato.” Alifafanua Bw. Mbalwe. Kuanzishwa kwa GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratinbiwa vizuri zaidi na iweze kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na wananchi wanaojishughulisha kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.
“Sekta inakuwa kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake.” Alifafanua Bw. Mbalwe. Amesema kuwa mwaka wa fedha unaoishia Jalai watafika bilioni 200 kutokana kwa miazi mitatu kuanzia Agasti hadi Desemba zaidi ya bilioni 100 zimepatikana. Amesema ajira zilizozaliswa Sekta ya michezo yakubahatisha Tanzania imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000. Mbalwe amesema kuwa GBT hadi sasa imesajili kampuni 91 za michezo ya kubahatisha. Amesema ongezeko la Mapato ya Serikali yatokanayo na Kodi ya biashara ya michezo ya kubahatisha yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na hiyo kutokana udhibiti wa michezo. Amesema ajira zilizozaliswa Sekta ya michezo yakubahatisha Tanzania imefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000. Aidha amesema sekta imefanikiwa kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira nchini.