Tanzania emblem

Gaming Board Of Tanzania

Ushering a New Era in the Regulation of Gaming Industry in Tanzania
GBT Logo

Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) yachangia pato la taifa zaidi bilioni 170 kwa mwaka

11 May, 2024
Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) yachangia pato la taifa zaidi bilioni 170 kwa mwaka

BODI YA MICHEZO YA KUBAHATISHA TANZANIA (GBT) YACHANGIA PATO LA TAIFA ZAIDI BILIONI 170 KWA MWAKA.

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini (GBT),James Mbalwe amesema bodi hiyo imefanikiwa kuchangia pato la Taifa kufikia Tsh. 170.43 bilioni kwa mwaka, kuongeza ajira kwa vijana na kuvutia uwekezaji wa kampuni 67 za kitaifa na kimataifa.

Mbalwe amezungumza hayo jijini Dar es salaam ya kuwa bodi hiyo inaadhimisha miaka 20 toka kuanzishwa kwakwe na lengo ni kukuza, kusimamia, kufuatilia na kudhibiti tasnia ya michezo ya kubahatisha nchini  ili kuhakikisha uadilifu, uboreshaji wa manufaa ya muda mrefu ya kijamii na kiuchumi na ulinzi wa umma kwa ujumla kwa kutekeleza sheria za michezo ya kubahatisha na kufuata kanuni zake.

Amesema GBT  inatoa leseni kwa waendeshaji wote wa michezo ya kubahatisha, kufanya ukaguzi endelevu pamoja na kuishauri serikali kuhusu masuala ya kodi ya michezo ya kubahatisha.

Naye Mwenyekiti wa shirikisho la makampuni ya kubeti nchini  Sabrina Msuya amesema kuanzia tarehe 21 kutakua na bonanza na kutoa msaada kwa wahitaji  katika kuadhimisha miaka 20 toka kuanzishwa kwakwe kama njai ya kurudisha kwa jamais yente uhitaji kutokana na mapatao yanayopatikana kwenye michezo hiyo ya kubahatisha.

NEWS LINK: Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania (GBT) yachangia pato la taifa zaidi bilioni 170 kwa mwaka - Millard Ayo